Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ameagiza watendaji wa Vijiji kupima maeneo yote ya vijiji ili kuepusha migogoro ya ardhi na uvamizi holela.
Mhe. Nguli ametoa agizl hilo wakati wa ziara yake katika cha kijiji Doma, Kitongoji cha Mtakenini, ziara hiyo iliambatana na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
DC Nguli amesema kuna baadhi ya wananchi wamevamia eneo la kijiji lenye ekari 450 huku wakijihusisha na uuzaji wa maeneo hayo, hivyo ameagiza watendaji wa vijiji katika Wilaya kupima maeneo yote ya vijiji kupitia kampeni ya tutunzane mvomero.
"...yapimwe maeneo ya kijiji yote ndani ya wilaya hii kuepuka kuyauza kiholela...tunayo kampeni ya tutunzane inapima maeneo pimeni...amesema Mkuu wa Wilaya.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.