Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ameiagiza Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini – TARURA Wilayani humo kuhakikisha kuwa wanafanya marekebisho miundombinu ya barabara ambazo zimeathiriwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Mhe. Nguli ametoa agizo hilo Mei 18, 2024 wakati akikagua barabara zilizoathiriwa na mvua katika Tarafa ya Mvomero ikiwa ni muendelezo kwa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi Wilayani humo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema barabara ya Makuyu kuelekea Kijiji cha Kibati ina umuhimu kwa uchumi wa Halmashauri na kwa wananchi kwa kuwa wanategemea barabara hiyo kusafirisha mazao yao kupeleka sokoni na pia barabara hiyo ni muhimu katika upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi wa Vijiji vya Kibati, Ndole, Maskati na vijiji vingine. Hivyo amewataka Mameneja wa TARURA na TANROADS kuhakikisha kuwa maeneo korofi yanarekebishwa.
“...hawa wananchi kilichokuwa kwao kikubwa ni mazao, usafiri na huduma za afya... anapokwama kwenye barabara amekuwa amekwama kila kitu...” amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, amewataka kuhakikisha kuwa Mkandarasi atakaye tekeleza zoezi la marekebisho hayo anakamilisha kwa wakati ili wananchi waendelee na shughuli zao kama ilivyokuwa awali.
Katika hatua nyingine, Mhe. Judith Nguli alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Wami Dakawa ambapo aliiagiza kamati inayosimamia ujenzi huo kuhakikisha kuwa mafundi wanakamilisha kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma za mama na motto.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.