Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amesitisha zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano ya kukabidhi eneo la kijiji kwa mwekezaji TANMANG QUARRIES ili kujiridhisha kama taratibu za kumpatia eneo hilo zilifuatwa.
Mhe. Nguli ametoa kauli hiyo Mei 28, 2024 wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Salawe ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi Wilayani humo.
Mkuu huyo wa Wilaya amechukua hatua hiyo baada ya kupata uthibitisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Hoza ambaye amekili kutoa eneo la machimbo ya madini bila ridhaa ya mkutano mkuu wa Kijiji hivyo ametumia nafasi hiyo kusitisha zoezi la kusaini mkataba huo ili kujiridhisha kama taratibu za umilikishaji ardhi zilifuatwa.
“...nasimamisha hati ya makubaliano vile vile ule mkataba ambao tanmang Quarries anataka kuingia na kijiji mpaka pale nitakapokwenda kijijini kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa...” amesema Mhe. Judith Nguli.
Imeelezwa kuwa kwa mujibu washeria ya ardhi ya mwaka 1996 imebainisha kuwa Serikali ya kijiji inuwezo wa kutoa ekari 50 za ardhi baada ya mkutano mkuu wa kijiji kuridhia.
Aidha, Mhe. Nguli amewataka wananchi kuwa watulivu kipindi hiki cha kufuatilia taarifa za makabidiano ya eneo hilo kupitia mkutano mkuu wa kijiji.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.