Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto, ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kata ya Mkindo, akisema kuwa hatua hiyo itaondoa changamoto ya umbali pamoja na msongamano wa wanafunzi katika shule jirani na kuongeza fursa za kielimu kwa vijana wa eneo hilo.
Akizungumza alipotembelea mradi huo Agosti 15, 2025, Mkuu huyo wa Wilaya amesema ujenzi wa shule hiyo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
“...kwenye ziara yangu miongoni mwa miradi iliyonifurahisha sana moja wapo ni huu katika kijiji cha Mkindo, mmefanya kazi nzuri sana..." amesema Mhe. Dotto.
Aidha, amewashukuru viongozi wa kijiji na kata kuhakikisha wananchi wanaendelea kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi kwa kuchangia nguvu kazi na kufanikisha ukamilishaji wa majengo kwa muda uliopangwa huku akisisitiza kuwa waendelee na ukamilishaji ili shule hiyo ianze kupokea wanafunzi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo ni zimetoka Serikali kuu ambapo zaidi ya shilingi milioni 528 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo. Ameongeza kuwa ujenzi huo unajumuisha vyumba nane vya madarasa, Jengo la utawala, Jengo la Tehama, Maabara mbili, maktaba pamoja na matundu ya vyoo, hata hivyo ujenzi umefikia asilimia 90 na matarajio ni kuwa hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2025 itakuwa imekamilika kwa asilimia 100.
Nao baadhi ya wananchi wa Mkindo wamemshukuru Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu, wakieleza kuwa shule hiyo itapunguza gharama na umbali wa wanafunzi kutembea kufuata elimu katika kata nyingine.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.