Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mnamo Aprili 26 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewaongoza Viongozi mbalimbali pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero.
Zoezi hilo la usafi limefanyika leo Aprili 23, 2024 likiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Said Nguya, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mkuu huyo wa Wilaya amesema zoezi hilo la usafi ni miongoni mwa miongozo iliyotolewa na Serikali kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo ziliungana kuunda Tanzania Aprili 26, 1964.
Aidha, ameeleza kuwa kuelekea maadhimisho hayo kutakuwa na mfululizo wa matukio mbalimbali yakiwemo mazoezi ya viungo na riadha, midahalo, pamoja na michezo mbalimbali.
“Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa letu”.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.