Mkuu wa Wilaya ya Mvomero amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka huduma ya madaktari bingwa kwenye maeneo ya wananchi huku akibainisha kuwa kitendo hicho kinawapa watendaji wa Serikali ujasiri wa kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali ya Dkt. Samia.
Mhe. Nguli ametoa shukrani hizo Juni 4, 2024 wakati akizindua Kliniki Tembezi ya Madaktari bingwa wa Rais Samia Wilayani Mvomero ambapo Madaktari hao wameweka kambi ya siku tano katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero wanatarajia kutoa matibabu ya kibingwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema wananchi wanachangamoto mbalimbali za kiafya hususan za kibingwa, hivyo Serikali ya Dkt. Samia imeamua kuchukua hatua ya kuwasogezea huduma hizo kwenye maeneo yao.
“…niendeleee kumshukuru Mhe. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anatuvesha nguo sisi wasaidizi wake kwa sababu tumekuwa tukipita sehemu mbalimbali tunakuta changamoto za wananchi ni kubwa upande wa kiafya…”amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Mhe. Nguli ametumia nafasi hiyo kuwa asa wananchi kuwapuuza watu wasiona mapenzi mema na Serikali ya Dkt. Suluhu Hassan kwamba haifanyikazi huku akibainisha kuwa Serikali hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha Sekta ya Afya.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kujikinga dhidi ya magonjwa ya tumbo, kuhara na kutapika kwa kutumia maji safi na salama kabla au baada ya kula, baada ya kutoka chooni, kuosha matunda na mbogamboga pamoja na kula chakula cha moto.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Dkt. Philipina Philipo amebainisha kuwa mwananchi wamekuwa na mwitikio chanya ambapo siku ya kwanza ya huduma za kibingwa wameandikisha wagonjwa 114, hivyo ameendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza katika hospitali ya Wilaya ili wapate huduma hizo.
Dkt. Philipina ameeleza huduma zitakazotolewa na madaktari bingwa ikiwa ni pamoja na huduma ya magonjwa ya wanawake, huduma ya magonjwa ya ndani, huduma za watoto na watoto wachanga, upasuaji na huduma za ganzi na usingizi.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake ambaye pia ni kiongozi wa msafara huo amesema watakuwepo Hospitalini hapo kwa muda wa wiki moja lengo ni kutoa huduma za kibingwa ili kuwapunguzia gharama ya kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa kama Muhimbili, KCMC, Benjamin Mkapa, Morogoro na maeneo mengine na huduma hizo zitatolewa katika Hospitali za Wilaya 185 hapa nchini.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.