Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto Agosti 14, 2025 ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata za Mgeta, Nyandira na Tchenzema ambapo amefurahishwa na utekelezaji wa mradi miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo amewapongeza wasimamizi wake huku akiwasisitiza wananchi kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa iliyokusudiwa.
Sambamba na hilo Mhe. Maulid Dotto amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwahudumia wananchi wa Wilaya hiyo akiongeza kuwa miradi hiyo inatatua changamoto za wananchi moja kwa moja.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa, Bweni moja na matundu 13 ya vyoo katika shule ya Sekondari Mgeta, Matundu ya vyoo katika Zahanati ya kijiji cha Kibaoni, pia amekagua na kuona shughuli za kikundi cha Twilose, Mradi wa matengenezo ya barabara ya Langali - Bumu - Mwarazi pamoja na matengenezo ya barabara ya Nyandira -Tchenzema.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.