Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli ameagiza usajili wa Shule Shikizi katika kijiji cha Mingo ukamilike haraka ili iweze kupokea wanafunzi kuanzia Januari 2026.
Agizo hilo limetolewa Machi 27, 2025 wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Mingo iliyolenga kutoa hamasa ya mapokezi ya mwenge wa uhuru 2025 pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza wananchi wa Kijiji hicho kwa kujitoa kujenga shule hiyo ambapo hadi sasa vyumba sita vya madarasa vimekamilika hivyo amemuagiza Kaimu Afisa Elimu ya Awali na Msingi kubadili matumizi badala ya kuongeza chumba cha darasa wajenge Vyoo ili shule hiyo isajiliwe na kupokea wanafunzi ifikapo Januari 2026.
"...hiyo ela yako hiyo ni vyoo, kuja kusajili hakuna kujenga tena boma hapa...mwakani mwezi wa kwanza shule ianze haya ni maagizo yangu..." amesema Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Gideon Shangweni amesema kuwa Halmashauri imepeleka idadi ya maboma yanayohitaji kumaliziwa kwa fedha kutoka serikali kuu kwa bajeti ya 2025/2026 ambapo kila shule yenye boma taarifa zake zimepelekwa Serikalini kwa ajili ya umaliziaji. Aidha, ameongeza kuwa jumla ya shule tatu ambazo zimechakaa zimetengewa bajeti ambapo shule ya msingi Mafuru, Chohero na Luale zitarekebishwa.
Awali Mwenyekiti wa Kitongoji cha Vianzi
akiwasilisha kero ya uwepo wa boma moja katika shule ya msingi Mwenge Kichangani amesema boma hilo lina zaidi ya miaka mitatu hivyo ameiomba Serikali kusaidia umaliziaji wa boma hilo huku akisema kuwa shule hiyo inajumla ya madarasa matano hadi sasa.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.