Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto ametembelea na kukagua Kikundi cha Melela Youth Group ambacho kinajihusisha na shughuli za usafirishaji abiria aina ya boda boda. Kikundi hiki kimepata mkopo wa Sh. 20,000,000, matarajio yao ni kununua gari aina ya Naoh kwa ajili ha kusafirisha abiria.
Aidha Mhe. Maulid Dotto ametoa wito kwa wakina mama wajikite kwenye mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri na kuwashauri waachane na mikopo kausha damù. Pia amekipongeza kikundi hicho kwa kuwa mfano wa kuigwa na kukitaka kiendelee kulipa ili kiweze kupatiwa tena mkopo.
Mwenyekiti wa kikundi hicho amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuanzisha utaratibu wa mikopo ya Asilimia 10 ambayo imewaweze kuwainua wananchi kiuchumi. Pia ameishukuru Halmashauri kwa kuwapatia elimu yq ujasiriamali na urejeshaji wa mikopo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.