Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli ametoa marufuku kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika Wilayani humo hususan wanaosimamia wakulima wadogo wa Miwa kusaini mikataba na Viwanda bila kuishirikisha Halmashauri kwa kufanya hivyo wanaharibu taswira ya vyama vya ushirika pamoja na kuwaingizia hasara wakulima.
Mhe. Nguli ametoa kauli hiyo Septemba 03, 2024 wakati akizungumza na wakulima wadogo wa miwa kutoka vyama vitatu vya ushirika vikiwemo TUCOCPRCOS LTD, MCOCOS LTD na DIKAMCOS LTD katika ukumbi wa mikutano wa Community centre uliopo katika Kata ya Mtibwa.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Nguli amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya wakulima hao ambayo yamechangiwa na mapungufu yaliyopo katika mkataba uliosainiwa kati vyama vya ushirika kikiwemo chama cha DIKAMCOS LTD.
Mapungufu yaliyotajwa katika mkataba huo ni pamoja na Halmashauri haijashirikishwa, mkataba huo umetumia lugha moja ya kiingereza lakini pia mkataba huo hauwapi nafasi wakulima wa miwa wa maeneo hayo kwenda kuuza miwa yao kwenye viwanda vingine. Hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku kwa viongozi wa vyama hivyo kusaini mkataba na kiwanda bila kuishirikisha Halmashauri ya Mvomero.
"...niagize kuanzia leo ni marufuku kufanya makubaliano pasipo kuishirikisha Halmashauri akaye fanya hivyo huo ni halali yangu...amesema Mkuu wa Wilaya.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.