Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amekema vikali wanaotumia fedha za Serikalia vibaya. Ameyasema hayo alipotembelea Shule ya Msingi Lugono na Shule ya Msingi Tangeni ambapo amezitaka Mamlaka husika kulifuatilia suala hilo. Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maagizo ya kuvunjwa kwa Kamati ya ujenzi ya Shule ya Tangeni na kuagiza wananchi wapewe taarifa kuhusu suala hilo, “TAKUKURU ifuatilie suala hilo kwa kufanya uchunguzi, Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri afanye ukaguzi wa fedha zote zilizoletwa na mradi wa BOOST na kusitisha matumizi ya “open cheque” kwa Shule zote mpaka watakapofanya marekebisho”.
Aidha Mkuu wa Wilaya akatoa maagizo ya kukamatwa kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lugono Shabani Mpili kwa tuhuma ya ubadhilifu wa fedha za Serikali. Pia aliagiza mamlaka za nidhamu imchukulie hatua za kisheria mwalimu huyo.
Alimpongeza Mwenyekiti wa Kijiji Ndg. Robert Selestine kwa kutoa taarifa mapema na aliwataka Walimu wawe wanatoa taarifa za ubadhilifu mapema wanapogundua kuna viashiria vya uhalifu na kuwataka kuzingatia maelekezo ya fedha za utekelezaji wa miradi.
Katika hatua nyingine Mhe. Diwani wa Kata ya Mzumbe Mhe. Godfrey Lumongolo alimwomba Mkuu wa Wilaya kufanya uhamisho wa Walimu ili kuepusha sintofahamu ambazo zinaweza kujitokeza mara kwa mara huku akimpongeza Afisa Elimu Wilaya kwa jitihada alizochukua awali kumhamisha Mwalimu huyo kutoka kituo chake cha awali. Pia Mhe. Diwani alionyesha kutofurahishwa na mwenendo wa Kamati ya Shule hiyo huku akishauri ijali zaidi maslahi ya wanafunzi ili kuongeza ubora wa taaluma Shuleni hapo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.