Katika kikao maalum cha tathmini ya maendeleo ya sekta ya afya Wilayani Mvomero kwa Mwezi Novemba 2024, Timu ya Usimamizi na Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) imepongezwa kwa jitihada zake za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pongezi hizo zimetolewa Novemba 20, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Mwl. Linno Mwageni wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ambacho kilienda sambamba na kukabidhi vyeti vya pongezi kwa baadhi ya wajumbe wa timu hiyo.
Mkurugenzi huyo ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji wa timu hiyo ambapo utendaji kazi huo umechangia kuleta mafanikio katika sekta ya Afya ndani ya Halmashauri hiyo huku akiweka msisitizo juu ya kusimamia miradi ya sekta ya afya ili ikamilike kwa wakati kuendelea kuwahuduma
"...najisikia amani kwa sababu kwanza mipango yenu mnayoipanga mnaitekeleza kwa wakati, sasa niwatie shime muendelee hivyo hivyo..." amesema Mwl. Linno.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa halmashauri, wananchi, na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha malengo ya serikali ya kuboresha huduma za afya yanafanikiwa.
Pamoja na pongezi hizo, Mwl. Linno ameelekeza CHMT kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa ya tumbo na kuhara hususan katika kipindi cha mvua ikiwemo kuwaelimisha wananchi kunawa mikono, kuchemsha maji pamoja na kuyatibu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Philipina Philipo wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya timu hiyo wameahidi kufanyakazi kwa bidii ili kuboresha utoaji wa huduma za afya katika Wilaya hiyo.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.