Mkuu wa mkoa mstaafu Brigedia Jenerali Mstaafu, Emanuel Maganga aliyefariki dunia katika Hospitali ya Jeshi ya Mirambo, Manispaa ya Tabora atazikwa nyumbani kwake Mvomero mkoani Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Philemon Sengati ameiambia Mwananchi Digital leo Ijumaa Januari 22, 2021 kwa njia ya simu kuwa marehemu ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Chabutwa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora atazikwa Mvomero kwa sababu ndiko alikojenga mji wake.
Marehemu Maganga alifikwa na mauti usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Jeshi Mirambo alikokimbizwa baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake mtaa wa Ipuli, Manispaa ya Tabora alikokuwa kwa shughuli za kifamilia.
Kwa mujibu wa Dk Sengati, mwili wa marehemu utahamishiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam utakakohifadhiwa wakati taratibu za kijeshi na maandalizi ya mazishi yakiendelea.Kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Lugalo kwa ndege maalum ya Jeshi, ibada fupi ya kumwombea na kumuaga marehemu itafanyika katika Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), mjini Tabora.
habari halisi: Mwananchi
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.