Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero limekutana Februari 09, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kwa ajili ya kujadili na kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027.




Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Ndg. Paulo Faty, amesema kuwa lengo la Baraza la wafanyakazi ni kushirikishwa katika maamuzi huku akiwataka wajumbe kuhakikisha kuwa wanaenda kueleza watumishi wengine yale yaliyojadiliwa katika kikao hicho.




Kwa upande wake Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo ameeleza vipaumbele saba (7) vya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 vikiwemo kuboresha huduma za elimu, kuboresha huduma za afya, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, kuwawezesha wananchi kiuchumi, kuimarisha huduma za ugani wa kilimo na ugani wa mifugo pamoja na kuendelea kusimamiana kuhimiza utunzaji wa mazingira.



Wajumbe wa Baraza walipata fursa ya kuchangia maoni na mapendekezo yaliyolenga kuboresha mpango huo, hususan katika maeneo ya kuongeza vyanzo vya ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Baada ya majadiliano, Baraza la Wafanyakazi lilikubaliana na kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027, hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero.





MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.