Halmashauri ya Wilaya Mvomero imekabidhiwa yaliyokuwa majengo ya Wakala wa Barara Nchini (TANROAD) yaliyopo Kijiji cha Mvomero wilayani Mvomero ili kuwa kituo cha Afya Mvomero tarehe 21/03/2019. Majengo yaliyokabidhiwa ni pamoja na Nyumba type one iliyokuwa ikitumiwa na Mhandisi Mkazi, Nyumba type two iliyokuwa ikitumiwa na Wahandisi wasaidizi, Nyumba za Multiple, Jengo la Ofisi, Jengo la Maabara, Uzio, Kisima cha maji na Matenki ya kuhifadhia maji, Mabanda ya kupaki magari, Mabanda ya walinzi, Banda la kufulia Nguo, na Jengo la choo cha Jumuia.
Akipokea hati ya makabidhiano, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven Kebwe amesema majengo hayo ni mazuri, na amesisitiza yatunzwe ili yadumu. Aidha katika kuimarisha utunzwaji wa majengo hayo, Dr. Kebwe amemuagiza meneja wa TANROAD kuweka vivuko maalum vya kupitishia Mifugo katika eneo hilo. Pia ameagiza huduma muhimu za Kituo cha Afya kama vile huduma ya upasuaji kama kigezo muhimu cha kituo cha Afya, viwepo katika kituo. Vile vile ameagiza thamani nyingi zilizokuwa katika majengo hayo zirudishwe ziweze kufaa katika uendeshaji wa kituo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mwl. Mohamedi Utaly amepokea hati ya makabidhiano ya majengo hayo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuyatunza ili yadumu. Pia amemsifia Mkurugenzi wa Halmashauri kuwa yupo makini na kazi yake na hivyo maagizo yatatekelezwa.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mvomero Ndugu. Florent Kyombo amekiri kupokea hati ya makabidhiano kwa niaba ya wananchi wa Mvomero na kuhakikisha kwamba yanatoa huduma inayostahili. Akiwasilisha risala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema majengo haya yanajitosheleza kuwa na huduma mbalimbali kama ifuatavyo; Wodi ya Akina Mama wajawazito, Wodi ya Watoto, Wodi ya wanaume, Wodi ya wanawake, Chumba cha upasuaji, Jengo la Mama baba na Watoto (RCH), Maabara, Bohari ya dawa, Chumba cha ufuaji, Chumba cha CTC, Chumba cha meno, Chumba cha wagonjwa wanje na Jengo la Utawala. Ameishukuru wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Wakala wa barabara (TANROAD) kuweza kukabidhi majengo haya katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambayo inapambana na vifo vya mama wajawazito na Watoto. Pia ameainisha changamoto mbalimbali zinazokabili idara ya Afya ikiwa ni pamoja na; Upungufu wa watumishi, Upungufu wa gari la kubebea wagonjwa pale inapotokea dharura kwa ajili ya kwenda hospitali ya Wilaya au Mkoa, Umeme mbadala kama vile jenereta au umeme jua (Solar), Mashine ya kufulia na Vifaa mbalimbali katika chumba cha upasuaji.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.