Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero leo Agosti 7, 2024 wametembelea banda la maonesho la Halmashauri hiyo katika Maonesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki 2024 yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere katika Manispaa ya Morogoro kupata elimu mbalimbali pamoja na teknolojia zinazotumika katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani hao, Mhe. Abdallah Botto ambaye ni Diwani wa Kata ya Diongoya ameipongeza Idara ya Kilimo kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo huku akisema kuwa elimu inayotolewa na wataalam wa Kilimo katika banda hilo ikatolewe kwa wakulima wengine ambao hawajapata nafasi ya kutembelea bandani hapo ili kuongeza uzalishaji wenye tija.
Aidha, Mhe. Botto amesema wao kama wawakilishi wa wananchi watahakikisha kuwa elimu hiyo inawafikia wananchi katika Kata zao.
Kaulimbiu ya maonesho hayo ya Nane nane 2024 inasema " Chagua Viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo endelevu ya sekta za kilimo, mifugo na uvuvi"
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.