Mnamo Tarehe 20 Februari, 2023 Timu ya Wajumbe 16 ikijumuisha Katibu Tawala Mkoa (RAS), Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji (W), Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri, Wakuu wa Idara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mipango na Uratibu na Maliasili na Mazingira, Afisa Mawasiliano Serikalini na Mtendaji wa Kata ya Dakawa, Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti TARI (3) na Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji UWAWAKUDA walifanya ziara ya kimkakati Tanzania Visiwani na kujikita katika maeneeo tofauti tofauti ikiwemo kukutana na baraza la wawakilishi
Ziara ilianza kwa kukaribishwa kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi ambapo taarifa ya Baraza kwa kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii ilikuwa ikiwasilishwa. Mheshimiwa Spika alitambulisha ujumbe wote na kuwakaribisha ndani ya Baraza hilo. Baada ya hapo wajumbe walipitishwa maeneo mbalimbali na kuelezwa mifumo mbalimbali ya uendeshaji wa Bunge la Baraza la wawkiloshi pia Wajumbe walitembelea shamba la viungo la Taasisi ya ZARI lililopo eneo la Kizimbani lenye ukubwa wa hekta 205 ambalo lilikuwa na viungo mbalimbali na shughuli za utafiti wa mbegu za mpunga na aina nyingine ya mazao (miti)
Ziara iliendelea kwa wajumbe kuonana na Mhe. Spika na kupokea taarifa ya Baraza ya Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii iliyotolewa maelezo mafupi na Mwenyekiti wa Kamati hiyo na baadae spika alitambua uwepo wa ujumbe huo na kutoa maelezo mafupi kuhusiana na uendeshaji mzima wa shughuli za Bunge na kuridhia ziara iendelee chini ya uratibu wa Wizara ya Kilimo ikiongozwa na Waziri wa Kilimo na Timu yake sambamba na wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati.
i) Timu ilianza ziara kwa kuwasili Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja na kupokea taarifa fupi ya Mkoa ikihusishwa idadi ya watu, majimbo na shughuli za kiuchumi. Mkuu wa Mkoa aliridhia ujumbe uendelee na ziara katika maeneo yaliyoandaliwa.
Timu ilitembelea Msitu wa Taifa wa Jozani ambapo wajumbe walipata maelezo kuhusu usimamizi wa msitu huo sambamba na uoto wa asili na wanyama waliopo katika msitu huo ambapo kuna mnyama aina ya kima ambae hapatikani katika msitu wowote duniani isipokuwa katika Msitu huo wa Jozani. Pia Kamati ilikwenda kutembelea shamba la mikoko lililopo eneo hilo ambapo Viongozi walipata fursa ya kupanda mikoko katika eneo hilo.
ii) Vilevile Timu ilipelekewa kwenye shamba la kilimo cha ndimu Bwajuu na kuona mfumo unaotumika katika uendeshaji wa kilimo hicho ambapo mfumo unaotumika ni wa umwagiliaji kwa misimu yote mwaka mzima.
iii) Wajumbe walitembelea shamba la mpunga lenye hekta 350 ambalo linatumika na wananchi kuzalisha mpunga.
iv) Baadae wajumbe walizuru eneo alikozaliwa na kukulia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan eneo la Kizimkazi na kupata Historia fupi ya safari yake ya kisiasa mpaka kuwa Mhe. Rais.
Katika hatu nyingine Wajumbe kwa kuongozwa na Katibu Tawala Mkoa waliendelea na ziara kwa kutembelea Baraza la Manispaa la Mjini na kupokelewa na Naibu Meya pamoja na Timu ya Wataalamu wa Manispaa hiyo ambapo, Afisa Mipango aliwasilisha taarifa fupi ikijikita kwenye vipaumbele vya:-
• Usafi na kupendezesha mji
• Kusimamia miradi ya maendeleo
• Kuboresha miundombinu ya wafanyabiashara
• Kuratibu na kusimamia masuala mtambuka
• Kuongeza vyanzo vya mapato
Mara baada ya taarifa hiyo na ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero uliwasilisha taarifa fupi na kuainisha fursa zilizopo Wilaya ya Mvomero na baadae timu zote mbili zilipitisha na kujengeana uzoefu katika maeneo mbalimbali yaliyoainishwa.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero aliomba kuwe na urafiki wa kujengeana uwezo baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Baraza la Manispaa la Mjini Unguja ambapo ombi hilo lilipita bila kupingwa.
Timu iliendelea na ziara katika maeneo ya Baraza la Manispaa Mjini Unguja na kuanza kutembelea maeneo ya udhibiti wa taka ngumu kutoka ngazi ya majumbani na kupelekwa kwenye kituo kidogo cha kukusanyia taka na baadae kutolewa kwenye kituo hicho na magari makubwa na kupelekwa eneo la dampo.
Baadae timu ilipelekwa eneo la uwekezaji wa maduka ya kisasa yapatayo 400 kwa awamu ya kwanza ya eneo la darajani (Zanzibar souk Market place), Mfumo wa uwekezaji huu ni baina ya Baraza la Manispaa na mbia yaani PPP ambapo makusanyo ni 75% ya mwekezaji na 25 ya Manispaa na mkataba ni wa miaka 20.
Vilevile wajumbe walipitishwa kwenye kanisa la kwanza la Anglikan ambapo pia biashara ya soko la watumwa ilifanyika eneo hilo, timu ilipata ufafanuzi na maelezo mbalimbali ya kihistoria.
Pia timu ilitembelea soko la samaki la Malindi ambapo iliona soko ambalo linatumia umeme unaozalishwa.
.
Na katika kuhitimisha ziara hiyo wajumbe walitembelea Kusini Unguja ambapo ilifika katika Halmashauri ya Kusini na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja na Timu ya Wataalam ambapo ilipokea taarifa fupi ya Halmashauri hiyo. Baada ya Taarifa hiyo timu ilienda kwa kutembelea ufugaji wa kuku kwa njia ya Kisasa katika eneo la Pwani Mchangani na kuona ufugaji wa kuku wanatotolesha mayai ya kisasa na baada ya kuona miradi hiyo Timu ilipata nafasi ya kufanya majumuisho pamoja na Wataalam wa Wizara ya Kilimo na Wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.