Mwenyekiti Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mvomero Bibi Rachael Kingu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo amekabidhi kadi ya Bima kwa mtoto Omary Idd Kiyondo wa Kijiji cha Salawe, Kata ya Kibati, Tarafa ya Mvomero iliyotokana na Harambee kutoka kwa Wanawake wa Wilaya ya Mvomero iliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kiwilaya yalifanyika tarehe 05 Machi, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Zoezi hilo la kukabidhi Bima hiyo limefanyika Mei 30, 2025 nyumbani kwa mtoto Omary Idd Kayondo katika kijiji cha Salawe.
Akizungumza wakati akikabidhi Bima hiyo, Bibi Rachael Kingu amesema kuwa Wanawake wa Wilayani ya Mvomero waliguswa na changamoto ya mtoto huyo hivyo walifanya harambee ambapo walipata zaidi ya shilingi 300,000 huku akibainisha kuwa wameshirikisha wadau mbalimbali ambao wamewezesha kupatikana kwa bima kwa ajili ya matibabu yake.
Aidha, amewashukuru Wanawake wote pamoja na wadau ambao wamefanikisha kupatikana kwa bima na nauli kwa ajili ya matibabu huku akiwasisitiza wazazi wa mtoto huyo kumpeleka mtoto akapate matibabu katika hospitali waliyoelekezwa na wataalam.
Kwa upande wake, Baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Idd Mwinjuma Kiyondo ameishukuru Serikali kwa msaada huo wa bima akibainisha kuwa awali alishindwa kumudu gharama za matibabu kutokana na kukosa fedha lakini kupitia msaada huo mtoto atapatiwa matibabu.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.