Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Twaha Kilango amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli kwa juhudi zake kwa kushirikiana na wananchi kudumisha amani Wilayani humo.
Akitoa pongezi hizo Juni 28, 2024 Shekhe huyo amesema Mvomero ya sasa imetulia hakuna migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na matukio mengine ambayo yalikuwa yanaipa sifa mbaya wilaya hiyo.
"...utulivu uliopo Mvomero si kawaida yake kwa wakati huu...Mvomero sasa hivi inaamani inautulivu wa hali ya juu..." amesema Shekhe Twaha.
Aidha, Shekhe Twaha amesisitiza ushirikiano kati ya wananchi, viongozi wa serikali na dini ili kuendelea kudumisha amani hiyo. Pamoja na hayo S
hekhe huyo ameshauri uandaliwe mkutano wa viongozi wa dini zote, wazee wa kimila na wazee maarufu lengo kujadili masuala mbalimbali ya kijamii.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.