Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wananchi wa Kijiji cha Kambala Kata ya Mkondo Wilaya ya Mvomero kuacha migogoro ya ardhi kwani inazolotesha maendeleo ya Kijiji hicho.
Mhe. Malima ameyasema hayo mapewa wiki hii wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambala kwenye Mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuhamasisha maendeleo na kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo amesema ameshangaa kwani nini wafugaji wanagombana na wakulima wakati wanatakiwa washirikiane kwani kinyesi cha ng’ombe ni samadi mkulima anaihitaji.
Mhe. Malima ameahidi kupeleka timu ya Wataalam wa ardhi ikiongozwa na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Morogoro Bw. Frank Minzikutwe ili kwenda kuweka michoro ya maeneo yenye migogoro na kumaliza migogoro hiyo.
Pia aliwataka wafugaji kuacha kupeleka watoto wadogo kuchunga kwenye mashamba ya watu hali inayopelekea kuwepo kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji. Ili kuweza kukabiliana tabia hiyo ya wafugaji Serikali ya Mkoa ipo na mkakati wa kutunga Sheria ndogo kukomesha uingizaji wa mifugo katika mashamba ya wakulima.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewashauri wafugaji katika Kijiji cha hicho na Mkoa mzima kwa ujumla kufanya ufugaji wenye tija ili kuinua uchumi wao. Matarajio yake ni kuona wanafuga kibiashara na kuwa mfano kwa wafugaji wengine hapa nchini. Aidha wenye mifugo mingi wahakikishe wanakuwa na eneo la malisho na kisima kwa ajili ya maji ya mifugo yao
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.