• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MVOMERO YAPONGEZWA KURITHISHA ELIMU YA MAZINGIRA KWA WATOTO

Posted on: April 20th, 2024

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndg. Godfrey Eliakimu Mzava ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kuwarithisha watoto elimu ya utunzaji wa mazingira ili waweze kuwa mabalozi wazuri katika jamii juu ya utunzaji wa mazingira ambapo imeelezwa kuwa Wilaya hiyo imeanzisha klabu 57 zinazotoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule za awali na msingi.

Ndg. Godfrey Mzava ametopongezi hizo Aprili 20, 2024 wakati mwenge wa Uhuru ulipotembelea shule ya Msingi Manyinga kwa ajili ya kukagua na kuona maendeleo ya mradi wa utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule za awali na msingi shuleni hapo.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amesema watoto wakipatiwa elimu ya utunzaji wa mazingira itaisaidia jamii kuwa na mabalozi wazuri na wazalendo katika kutunza mazingira kwa vizazi vya sasa na baadaye.

“…ukiendelea kuwalea watoto hawa wadogo wakatambua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira watakuja kuwa watu wakubwa na watakuwa mabingwa wazuri sana wa masuala ya utunzaji wa mazingira…”amesema Ndg. Godfrey Mzava.

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopata athari za mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na shughuli zisizofuata uendelezaji na utunzaji wa mazingira zikiwemo uchomaji wa misitu, kilimo, ufugaji, kilimo na shughuli kama za viwandani.

Nao wanafunzi waliopata elimu ya utunzaji wa mazingira shuleni hapo akiwemo Jackline Eliaba mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Manyinga amesema suala la upansaji miti ni la kila jinsia yaani wanawake kwa wanaume huku akibainisha kuwa ushiriki wa jinsia zote katika upandaji miti na usafi wa mazingira utasidia kukakabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa upande wake Jenifa Solomon mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo amebainisha kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule 57 zinazotoa elimu ya utunzaji wa mazingira Wilayani humo. Aidha, kwa niaba ya wanamazingira wa Wilaya hiyo amewaomba wananchi Wilayani humo kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hapa nchini mwezi Oktoba, 2024.

Mwenge wa uhuru umemeliza mbio zake Wilayani Mvomero ambapo umekagua, kuona, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi nane yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 1.4.

MWISHO.

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO KUENDELEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA GoT-HoMIS KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

    May 09, 2025
  • MOROGORO YAJA NA MKAKATI KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI

    May 01, 2025
  • DC NGULI ATIMIZA AHADI YA KUGHARAMIA MATIBABU YA KIJANA RAMADHANI MOHAMED

    April 28, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUWAPUUZA WANAOCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI

    April 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.