Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okash akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ,pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri na wataalam wa Wilaya leo wamejumuika pamoja katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika Kituo cha Afya Mlali kilichopo Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewahimiza wananchi wa Mvomero kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ili kuenzi kwa vitendo kumbukizi ya siku ya Mashujaa waliojitoa kufa na kupona kupigania Uhuru wa nchi hii .
Pia Mhe. Halima Okash ameendelea kuwa kukumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 23 Agosti katika zoezi muhimu la Sensa linalotarajia kufanyika nchini kote.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.