Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa ameongoza ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa Makarani Waongoza Wapiga Kura, akisisitiza umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na maelekezo yote yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa amani.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Oktoba 25, 2025 yaliyofanyika katika ukumbi wa Community Centre uliopo Tarafa ya Turiani Msimamizi huyo wa Uchaguzi amesema kuwa jukumu la Makarani ni muhimu sana katika kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa uwazi na uadilifu, hivyo ni lazima wazingatie maadili ya kazi na kuepuka upendeleo wa aina yoyote.
“...mnategemewa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yote mtakayopewa..." amesema Bi. Mary Kayowa.
Aidha, Msimamizi huyo wa uchaguzi amewasisitiza makarani hao kutokuwa sehemu ya malalamiko kwani wao ndiyo taswira ya zoezi la uchaguzi.
sambamba la hilo, wakati akihitimisha mafunzo hayo katika ukumbi wa prof. Kuzilwa uliopo katika Kata ya Mzumbe, Msimamizi huyo wa uchaguzi amewataka kuzingatia suala la muda ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima huku akiwasisitiza kuwa na lugha nzuri kwa wapiga kura.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa ubora wa zoezi la upigaji kura linaanzia kwao kama waongoza wapiga kura kwa sababu wao ni kama kamati ya mapokezi kwani namna watakavyo wapokea wapiga kura itaathiri mchakato huo.
"Kura yako Haki yako, Jitokeze kupiga kura"
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.