Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha, kujua maeneo ya mipaka na kusikiliza kero za wananchi katika Kata na Vijiji vya Wilaya ya Mvomero, ambapo Oktoba 15, 2025 amefika Kijiji cha Salawe Kata ya Kibati akiwa ameambatana na Wataalam kutoka Halmashauri na Taasisi mbalimbali zilizomo ndani ya Wilaya ya Mvomero.
Katika mkutano huo wa hadhara, wananchi walipata fursa ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo tatizo la maji kutoka machafu na miundombinu mibovu ya maji inayosababisha ukosefu wa maji, kuharibika kwa barabara ya tembo - Diburuma na Mkandarasi hayupo eneo la kazi, migogoro ya ardhi kati ya Hoza na Pemba, Hoza na Kibogoji, Diburuma na Pandambili, Lusale (Kilindi) na Salawe (Kibati Mvomero). Huduma za Afya watoto na wazee i kuchangishwa fedha, kukatikakatika kwa umeme ambapo inapelekea uharibifu wa vifaa na upungufu wa watumishi.
Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Mhe. Dotto aliwataka Wataalam watoe majibu kwa hoja zilizowasilishwa mezani
Mtaalam kutoka RUWASA Ndg. Michael Mdoe alieleza kuwa mradi wa maji unakabiliwa kuwa na miundombinu chakavu, Serikali ipo katika harakati za kujenga mradi mkubwa wa maji Kibati katika Kijiji cha Kipangilo, Hoza, Salawe, Diburuma mkandara anasubiri kusaini mkataba.
Kuhusu suala la kukatika kwa umeme Meneja wa TANESCO ndg. Daniel Chaula alieleza kuwa Kijiji cha Kibogoji waya unaopeleka nishati umepata hitilafu hivyo aliwaomba wananchi wawe wavumilivu wataalam wanalifanyia kazi.
Suala la ubovu wa barabara Tembo mchafu - Pandambili mwakilishi Meneja wa TARURA Ndg. Pantaleo alieleza kuwa suala hilo limewekwa kwenye bajeti 2025/2026. Mkandarasi hayupo katika eneo la kazi kwasababu kulikuwa na changamoto ya fedha pamoja na barabara ya Salawe - Diburuma.
Mgogoro wa mipaka kati ya Hoza na Pemba Mkuu wa Wilaya aliomba apatiwe tathmini ya ripoti na maelekezo aliyotoa mtangulizi wake ili yeye aanzie hapo. Mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi na Mvomero watakaa pande zote mbili ili kulifanyia kazi
Wananchi walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika kusikiliza kero zao.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.