Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Mvomero kubuni vyanzo vya mapato ya ndani kupitia sekta ya kilimo.
Mhe. Malima ametoa kauli hiyo Juni 26, 2024 kwenye mkutano wa baraza maalumu la madiwani uliolenga kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa kupitia sekta ya kilimo pekee inaweza kuiongezea mapato Halmashauri hiyo mara dufu ya yale wanayokusanya sasa kutokana na kuwa na wingi wa fursa zilizopo kwenye sekta hiyo hususan uwepo wa mazao ya kokoa, karafuu na kilimo cha mpunga.
"...hii Halmashauri nataka itengenezewe mikakati ya kuzalisha mapato ya ndani yasiyopungua bilioni sita, bilioni sita na nusu ndani ya miaka mitatu kwa uzalishaji wa kilimo..." amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, ametaja sekta nyingine ikiwemo ya mifugo inamchango kwenye mapato ya Mvomero hivyo Halmashauri haina budi kuweka mikakati madhubuti ya kuiboresha ili kupata mapato zaidi.
Katika hatua nyingine, Mhe Malima amesema ili kuyafikia mafanikio tarajiwa watendaji wa Halmashauri wanatakiwa kushirikiana kuhakikisha kuwa Halmashauri inapata maendeleo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameeleza fursa zinazopatikana kwenye shina la mgomba akisema kuwa mgomba unazalisha nyuzi ambazo zinamatumizi mbalimbali huku akiwataka madiwani kuhamadisha vijana ili kujiajiri wenyewe.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.