Diwani wa Kata ya Dakawa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Yusuf Makunja, amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuhakikisha demokrasia inazingatiwa katika zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo tarehe 27 Novemba, 2024.
Akizungumza mapema hii leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Magengeni kilichopo Kata ya Dakawa, Mhe. Makunja amesema kuwa tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi huo yanaonyesha dhamira ya kweli ya Rais Samia ya kuimarisha misingi ya demokrasia.
"...tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuhakikisha demokrasia inazingatiwa, hakuna vurugu..." amesema Mhe. Makunja.
Aidha, Mhe. Makunja amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi bora watakaosimamia maendeleo ya maeneo yao.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura akiwemo Bw. Joel Kilongo na Bi. Zafarani Mtuli wakazi wa kitongoji cha CCM wamepongeza utaratibu mzuri wa zoezi la kupiga kura huku wakiwahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi wao.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.