Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Mhe. Christopher Maarifa leo Januari 29, 2025 ameongoza ufunguzi wa semina maalum kwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji pamoja na Watendaji wa Vijiji kutoka tarafa za Mlali na Mgeta, semina hiyo inafanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mzumbe.
Akizungumza katika semina hiyo, Mhe. Maarifa amewataka viongozi hao wa serikali za mitaa kuhakikisha wanazingatia ushirikiano wa karibu na wananchi, watendaji wa vijiji, kata na ngazi nyingine za uongozi ili Halmashauri hiyo isonge mbele.
Aidha, amewakumbusha Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kuwa ni wajibu wao kusimamia amani na utulivu katika maeneo yao, pamoja na kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi kwa njia shirikishi.
Sambamba na hilo amewataka kubuni miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ambayo inatekelezeka ili ilete tija iliyokusudiwa.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.