Siku ya Mtoto wa Afrika ni siku inayoadhimishwa kila mwaka barani Afrika Tarehe 16 juni kuwaenzi mashujaa watoto waliokufa kwa ajili ya kudai haki yao ya kuendelezwa kielimu bila ubaguzi. Hii iliwekwa na Umoja wan chi za Afrika mnamo mwaka 1991. Kuanzia hapo maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika nchi wanachama kwa kufanya tathmini kuhusu hali ya utoaji wa haki ya mtoto na huduma zinazohusu malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, maadhimisho hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi ya Mvomero ikishirikisha wadau na viongozi mbalimbali wa Kiwilaya huku kauli mbiu ikiwa “Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali” ambao umeweka mahususi mwaka huu kwa kuwa idadi kubwa ya watoto wanatumia mitandao katika karne ya 21.
Katika kufanya maadhimisho hayo, vikundi mbalimbali vya Sanaa vilipita na ujumbe mbalimbali huku watoto wakibeba mabango mbalimbali yenye kubeba ujumbe wa kaulimbiu katika kufikisha ujumbe kwa hadhira na jamii husika.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.