MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO YAPAMBAMOTO.
Maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yamepambamoto Wilayani Mvomero ambapo Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Siasa pamoja na wananchi Wilayani humo wameungana na Watanzania wengine katika dua ya kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dua hiyo ya kuliombea Taifa imefanyika leo Aprili 22, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Judith Nguli.
Mwenyekiti wa Maandalizi ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Said Said ametoa ratiba ya matukio mbalimbali yatakayofanyika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Shereha za Muungano ambayo uhadhimishwa kila mwaka Aprili 26.


Matukio yaliyotajwa kufanyika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ni pamoja na dua ya kuliombea Taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imefanyika leo Aprili 22, shughuli ya usafi katika Hospitali ya Wilaya ambapo usafi huo utafanyika Aprili 23, tarehe 24 kutakuwa na mazoezi ya viungo, 25 Aprili kilele cha shughuli mbalimbali zilizofanyika kuelekea siku ya maadhimisho katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mzumbe.


Ikumbukwe kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuunda Tanzania mnamo Aprili 26, 1964 maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda na kaulimbiu isemayo “Miaka 60 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa letu”.

MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.