Kuundwa kwa jukwaa la Mnyororo wa thamani wa chakula Wilayani Mvomero kuna tarajiwa kuwa mkombozi wa changamoto za wakulima, wafugaji na wavuvi kwani watakuwa na uwezo wa kupata suluhisho la changamoto hizo.
Hayo yamebainishwa Julai 25, 2024 na Mwakilishi wa Shirika la Helvetors Bi. Agness Mahembe wakati wa kikao cha wadau wa Jukwaa la mnyororo wa thamani wa chakula kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Bi. Agness Mahembe amesema lengo la Jukwaa hilo ni kuwakutanisha wadau hao kujadili changamoto mbalimbali na fursa ambazo zinaweza kuwa suluhisho la jukwaa hilo kwenye shughuli za kilimo na ufugaji.
Aidha, amesema kuwa wadau hao kwa kushirikiana na Afisa kilimo wa Halmashauri hiyo wameunda rasimu ya Katiba ili kuwezesha jukwaa hilo kuwa endelevu.
Awali Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bi. Ruth Mazengo ameeleza faida ya uwepo wa jukwaa ikiwa ni pamoja na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umewasaidia wakulima kuuza mazao yao kupitia mfumo huo. Aidha, amebainisha kuwa kuna baadhi ya mazao ya kimkakati kama vile Kakao, ufuta, kahawa na iriki yamelengwa kuuzwa kwenye mfumo huo.
Nao baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho akiwemo Bw. Athuman Kipula amesema mfumo wa Stakabadhi ghalani ni mkombozi kwa mkulima lakini wakulima wengi hawana elimu juu ya mfumo huo huku akiomba wataalamu wa kilimo kutoa elimu kwa wakulima.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.