Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto ameshiriki dua maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika Oktoba 24, 2025 katika Msikiti wa Rahma uliopo katika Tarafa ya Turiani akisisitiza kuwa amani ni tunu adhimu ambayo kila Mtanzania anapaswa kuilinda na kuipa kipaumbele.
Akizungumza katika dua hiyo, Mhe. Dotto amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa nchi yenye amani na umoja, hivyo ni wajibu wa kila raia kuhakikisha hali hiyo inaendelea kudumu hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu 2025 wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani na kwamba amani hii iliyopo idumishwe kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameendelea kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba, 2025 ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Dua hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa viongozi wa dini pamoja na uongozi wa Kiwanda cha sukari Mtibwa huku ikihudhuriwa na viongozi wa dini wa Wilaya ya Mvomero, watumishi wa umma, pamoja na wananchi ambapo walitumia nafasi hiyo kuomba baraka, umoja na uongozi wenye hekima kwa Taifa.
Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu wa Kiwanda cha sukari Mtibwa Bw. Shani Mligo kwa niaba ya uongozi wa kiwanda hicho amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya kijamii na kiimani, wakiahidi kuendelea kuliombea Taifa na kuhimiza amani na matendo mema miongoni mwa wananchi.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.