Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto Oktoba 16, 2025 amemendelea na ziara yake ya kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Lubungo Kijiji cha Kimambila na Kata ya Mzumbe Kijiji cha Changarawe. Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ameambatana na Wataalam wa Halmashauri na Taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wilaya ya Mvomero ambapo changamoto mbalimbali zimeibuliwa na wananchi.
Katika mkutano huo wa hadhara, wananchi walieleza kero zinazowakabili katika Vijiji vyao wakianza na Kata ya Lubungo changamoro ni tatizo la wanyama wakali na waharibifu (tembo na fisi), ukosefu wa ofisi ya Kijijini cha Kimambila kilichokuwepo kimepitia na nguzo A umeme, tatizo la umeme, ukosefu wa maabara, nyumba za walimu (Kimambila), ubovu wa barabara Lugala - Lukobe, wanaomba wajengewa Kituo cha Polisi, Polisi jamii hawana vitambulisho na vitendea kazi, ukosefu wa Zahanati, Vitongoji 4 havijafikiwa na umeme, wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima, ombi la kujengewa hosteli kwa watoto wakike, uhaba wa vitabu, uboreshaji wa viwanja vya michezo uliokuwepo umepitia na nguzo za umeme na mpaka kati ya Kijiji chha Kimambila na Lukobe.
Kwa upande wa Kata ya Mzumbe Kijiji cha Changarawe changamoto zilikuwa miundombinu mibovu ya barabara, ukosefu wa Kituo cha Afya, uhaba wa maji, wananchi wametakiwa kuhama nyumba zao kupisha mkondo wa maji, kuvamiwa kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya makaburi na ukosefu wa umeme na maji katika Kijiji cha Ngole.
Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Mhe. Dotto aliwataka Wataalam watoe majibu kwa hoja zilizowasilishwa mezani pia aliahidi kushirikiana na viongozi wa Halmashauri, Vijiji na Taasisi husika kuhakikisha changamoto zao zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka. Alisisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha maisha ya wananchi wa mvomero kupitia utatuzi wa migogoro, uboreshaji wa miundombinu na upanuzi wa huduma za kijamii.
Wananchi walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika kusikiliza kero zao moja kwa moja na kuonesha matumaini kuwa hatua stahiki zitachukuliwa ili kupunguza changamoto wanazokabiliana.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.