Wiki ya Chanjo imezinduliwa Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, kwa chanjo 172 kutolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Akizindua zoezi la Chanjo katika Zahanati ya Kata ya Dakawa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewatoa hofu wazazi wenye wasiwasi kuhusu usalama wa Chanjo hizo, kwamba ni ziko salama na wajitokeze kwa wingi kupeleka watoto katika vituo vya kutolea Chanjo.
Lakini pia DC Judith Nguli ameeleza kuwa watoto wadogo ni rahisi kunyemelewa na magonjwa mbalimbali hivyo ni muhimu wapatiwe Chanjo ili wawe salama katika hatua za ukuaji.
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Daktari Alex Mnzava Watoto wanaotarajiwa kunufaika na huduma ya Chanjo ndani ya Wiki hii ni 6,770 ambao wana umri wa chini ya miaka mitano, ilhali watoto wengine 1,220 waliochelewa kupata Chanjo mbalimbali wataendelewa kufikiwa na na huduma hiyo.
Daktari Alex Mnzava ameongeza kuwa , katika Wiki hii ya Chanjo, watoto watakaopatiwa Chanjo pia, watapatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Malaria.
Jumla ya Chanjo zilizochanjwa katika Siku ya Uzinduzi ni 172 ambapo kati ya hizo, Chanjo ya Surua ya kwanza watoto waliochanjwa ni 65 na Surua ya Pili watoto waliochanjwa ni 67, wakati Chanjo ya Ugonjwa wa Polio, watoto waliochanjwa Polio ya Kwanza ni 13 na waliochanjwa Polio ya Pili 27”.
Aidha Chanjo nyingine itayotolewa ni Chanjo ya Mlango wa Shingo ya kizazi kwa watoto wa kike.
Wiki ya Chanjo imeanza tarehe 24 na inatarajiwa kukamilika tarehe 29 Mwezi wa April Mwaka 2023.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.