Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bibi Loema Peter amemkabidhi ofisini Ndg. Paulo Francis Faty ambaye alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita. Ndg. Faty amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua tena kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero pia ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na mtangulizi wake Bibi. Loema Peter.
Naye Bibi. Loema ametuma salamu za shukrani kwa viongozi mbalimbali, watumishi na wananchi kwa ushirikiano waliompatia kwa muda wote wa uongozi wake ndani ya Wilaya ya Mvomero.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya hiyo yakiwa yamehudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Divisheni za Utumishi na Utawala, Mipango na Uratibu na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Sheria, Fedha na Uhasibu na Ukaguzi wa Ndani.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.