• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

WILAYA YA MVOMERO NA HIFADHI YA MIKUMI WASHAURIANA KUTANGAZA FURASA ZA UWEKEZAJI

Posted on: August 17th, 2023

Wilaya ya Mvomero kwakushirikana na Hifadhi ya Taifa Mikumi wamepanga kuanzisha mkakati wa kuhakikisha wanatangaza fursa ya Uwekezaji katika maeneo yaliyoko jirani na Hifadhi kwakuweka vivutio vya kitalii ili kupunguza ongezeko la Wanyama waharibifu wa mazao na vifo vya binadamu.

Hayo yamezungumzwa hapo jana katika kikao Cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi za Hifadhi ya Taifa Mikumi kikihusisha pande zote zote mbili kwa upande wa Wilaya Mvomero uliwakilishwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya Judith Nguli,Kamati ya Usalama,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Yusuf Makunja ,Mkurugenzi Mtendaji na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri na kwa upande wa Hifadhi uliwakilishwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ignas Gara na Afisa Mwandamizi wa Hifadhi Herman Baltazary, lengo kuu ni kuangalia namna sahihi ya kuweka mkakati wa kutangaza fursa ya Uwekezaji katika maeneo yaliyoko jirani na Hifadhi husasani katika Vijiji vya Doma na Maharaka kuwa fursa ya Uwekezaji kwa kuweka vivutio vya kitalii .

Akizingumza katika kikao hicho Mhe. Mkuu wa Wilaya amewashukuru Viongozi wa Hifadhi kwa kuweza kuona fursa hiyo na kujumuika kwa pamoja kuandaa mpango-mkakati huo na kushirikisha uongozi wa Wilaya ili kuwa kitu kimoja kuandaa fursa hizo za uwekezaji katika maeneo hayo yanayopakana na Hifadhi kwa kufanya hivyo kutaweza kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo kuepukana na wanyama waharibifu lakini pia kutawawezesha wananchi hao kujipatia kipato kwa kulima mazao kama ufuta lakini pia kuwekeza katika shughuli za biashara na Utamaduni.

Mhe. Judith Nguli amewata wananchi hao kujiandaa kikamilifu kuchangamkia fursa hiyo kwani kwa mpango uliopo sasa eneo la Doma ndipo litakuwa lango kuu la kuingilia Hifadhi ya Taifa Mikumi mara baada ya Serikali kusaini makubaliano  kuanzia mwezi wa tisa kuanza ujenzi wa geti. Ujenzi huo utaanza na shughuli zote zote za kibiashara zitahamia katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuf Makunja amesema kuwa mpango huo utaunufaisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa kwanza kwa wananchi kuepukana usumbufu wawanyama waharibifu ambao wamekuwa kero kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo kiasi kwamba wamekuwa wakisababisha vifo kwa wanananchi lakini pia imekuwa fursa ya wananchi hao Sasa kujipatia kipato kwa kulima mazao ya kibiashara kama vile ufuta lakini kuwekeza katika shughuli za kibiashara kama vile kujenga mahoteli na kufanya shughuli za kiutamaduni

Aidha Mwenyekiti huyo amewataka Wataalam kuchangamkia fursa hiyo haraka iwezekanavyo kwa kufanya tathimini ya kina na kuandaa mchoro utakaoonyesha namna gani watapanga kisasa jinsi ya kutangaza eneo hilo kwa kuweka vivutio vya kitalii na hivyo kuwezesha Halmashauri kupata mapato kutoka eneo hilo .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema yeye pamoja na timu yake wameyapokea maelekezo hayo na watayafanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa kuandaa mpango kazi utakaoonesha namna gani shughuli zitakavyoendeshwa katika eneo hilo na kuuwasilisha katika kamati husika ili shughuli nyingine ziweze kuendelea.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi Ignas Gara amesema baada ya kilimo cha muda mrefu kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo wao kama hifadhi wameamua kuja na mpango huo kwa kuhakikisha kwanza wanaitangaza hifadhi hiyo ya Mikumi lakini pia wanawawezesha wananchi walioko jirani na maeneo hayo na Halmashauri kuweza kujipatia kipato.

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO KUENDELEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA GoT-HoMIS KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

    May 09, 2025
  • MOROGORO YAJA NA MKAKATI KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI

    May 01, 2025
  • DC NGULI ATIMIZA AHADI YA KUGHARAMIA MATIBABU YA KIJANA RAMADHANI MOHAMED

    April 28, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUWAPUUZA WANAOCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI

    April 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.