• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

RAS MOROGORO AENDELEZA KAMPENI YA "JISOMESHE NA MKARAFUU" KUWAWEZESHA WANAFUNZI KIUCHUMI

Posted on: March 14th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameendelea na kampeni ya Jisomeshe na Mkarafuu Wilayani Mvomero, ikiwa na lengo la kuwawezesha wanafunzi kiuchumi kupitia kilimo cha mkarafuu ambapo leo Machi 14, 2025 amegawa miche ya mikarafuu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari Kipera na Homboza.


Akizungumza wakati wa zoazi la ugawaji wa miche hiyo, Dkt. Mussa amesema Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameanzisha kampeni hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwaandaa vijana kwa maisha ya baadaye kwa kuwawezesha wanafunzi hao kujiendeleza kimasomo kupitia zao hilo.


Aidha, ameongeza kuwa miche hiyo wanapewa wanafunzi wakapande katika maeneo yao na si maeneo ya shule huku akisema kuwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza atapewa miche 10 akisisitiza kuitunza ili iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.


"...nyie wanafunzi wa form one, tunataka kila mwanafunzi mmoja leo hii, tumuachie miche ya mikarafuu kumi... miche hii isiwe mali ya shule mkaipande kwenu..." amesisitiza Dkt. Mussa


Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo, kwa sasa bei ya kilo moja ya karafuu ni shilingi 20,000/= hivyo, mche mmoja una uwezo wa kuzalisha kilo tano huku akisema kuwa kwa miche hiyo 10 itazalisha kilo 50 ambazo ni sawa na shilingi 1,000,000/= hivyo, wanafunzi wataweza kupata kipato na kusaidia gharama za masomo yao hapo baadaye


Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rozaria Rwegasira amesema kuwa kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, imeendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na sasa ipo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, huku akiwataka wanafunzi kuipokea kampeni hiyo ambayo itawasaidia kutimiza ndoto zao.


Naye, Mwl. Isakwisa Asesisye akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero amemshukuru Katibu Tawala huyo kwa kuanzisha kampeni hiyo katika Halmashauri hiyo huku akisema kuwa Halmashauri hiyo ina jumla ya shule za sekondari 37 ambapo kwa kuanzia kampeni hiyo imeanza kwa shule za Homba na Kipera.


MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO YAWEKA MIKAKATI YA KUFANYA VIZURI KATIKA KIPENGERE CHA USAFI WA MAZINGIRA

    August 20, 2025
  • ZOEZI LA UTOAJI FOMU ZA UTEUZI LAENDELEA KUSHIKA KASI

    August 20, 2025
  • UTOAJI WA FOMU ZA UTEUZI

    August 19, 2025
  • DC MAULID DOTTO AAHIDI KUTAFUTA ENEO KWA AJILI YA MASHINDANO YA MAGARI

    August 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.