• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MVOMERO YAENDELEA KUTENGA FEDHA KUTEKELEZA AFUA ZA LISHE, KUTOKOMEZA UTAPIAMLO, UDUMAVU

Posted on: December 15th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha afya bora kwa watoto, kina mama wajawazito na jamii kwa ujumla, pamoja na kutokomeza tatizo la utapiamlo na udumavu.


Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Lishe ya Wilaya kilichofanyika leo Disemba 15, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Paulo Faty amesema halmashauri imejipanga vyema kwa kutenga bajeti maalum ya lishe kila mwaka, sambamba na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa afua huzo katika ngazi ya kata na vijiji.


Amesema miongoni mwa mikakati iliyowekwa ni kuendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa jamii, kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubisho, kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na kuhimiza usafi wa mazingira ili kuzuia magonjwa yanayochangia utapiamlo.


Naye, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Dkt. Phillipina Phillipo amesema kikao hicho kimelenga kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya kwanza kipindi cha Julai - Septemba 2025.


Kwa upande wake Afisa Lishe wa Wilaya Bi. Niyonzima Bwenzi amesema kuwa kwa robo ya kwanza Halmashauri ilipanga kutoa kiasi cha shilingi milioni 19,698,750 ambapo fedha zilizotolewa ni shilingi milioni 36 ambayo ni sawa na asilimia 184. ameongeza kuwa kupitia kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe jumla ya watoto 56188 walipatiwa Vitamini A kati ya watoto 52840.


Akieleza hali ya utoaji wa chakula shuleni kwa shule za Sekondari Bw. Jaribu Marambugi akimuwakilisha Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari amesema Wilaya hiyo ina jumla ya shule za Sekondari 34 zenye wanafunzi 20171 ambapo kati yao wanafunzi 12506 sawa na asilimia 62 wanakula shuleni.


Kwa upande wa Divisheni ya elimu ya Awali na Msingi Bi. Aziza ameeleza kuwa idara imetenga kiasi cha shilingi milioni 1,600,000 kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe kwa shule za msingi katika Wilaya hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MKUTANO WA BARAZA LA KATA ROBO YA PILI OKTOBA - DISEMBA 2025/2026

    January 29, 2026
  • FURSA ZA UWEKEZAJI ISIWE CHANZO CHA MIGOGORO YA MIPAKA YA VIJIJI, VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMA IMARA KUIMALIZA

    January 28, 2026
  • MIPANGO, BAJETI ZA HALMASHAURI ZIENDANE NA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 - RC MALIMA

    January 27, 2026
  • DC MVOMERO ALIPONGEZA SHIRIKA LA SAWA KUJENGA MADARASA YA SHULE SHIKIZI, AAGIZA MCHAKATO WA USAJILI UANZE MARA MOJA

    January 23, 2026
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.