• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

Mkuu Wa Wilaya Apokea na Kugawa Vifaa Vya Msaada Kwa Waathirika wa Mvua na Upepo mkali Vijiji Vya Kipera na Kinyenze

Posted on: January 14th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh.Albinus Mugonya,amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kujenga nyumba imara na zenye ubora ili kukabiliana na majanga makubwa kama vile mvua,na upepo mkali pindi yanapojitokeza.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo hapo jana alipokuwa akipokea na kugawa vifaa vya msaada vilivyotolewa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo na Benki ya NMB kwa ajili ya wananchi walioathirika na maafa ya mvua na upepo mkali, yaliyotokea hivi karibuni katika vijiji vya Kipera na Kinyenze vilivyopo katika Kata ya Mlali,Tarafa ya Mlali na kuacha jumla ya Kaya sabini na sita (76) zikiwa hazina mahali pa kuishi.

Mkuu wa Wilaya amesema ni vyema wananchi kujenga utamaduni wa kujenga nyumba bora na imara ‘’Wananchi wanatakiwa kujenga nyumba imara ili kukabiliana na majanga kama haya yaliyojitokeza,kwani wangejenga nyumba zenye msingi imara haya yote yasingejitokeza’’ alisema.

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kuvigawa kwa waathirika hao ni Unga Kilo 764, Maharagwe Kilo 100 na Chumvi Kilo 60.Wakati huo benki ya NMB imekabidhi Magodoro 54,Mashuka 108 na Mchele Kg 540 pamoja na Mafuta lita 160,na Sukari Kilo 110.

Mkuu wa Wilaya amewashukuru wadau hao kwa kuona umuhimu wa jambo hilo na kuwataka walengwa kuvigawa vifaa hivyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa bila upendeleo wa aiana yoyote pia ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia kwani waathirika wanahitaji kuendelea kusaidiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Ndugu Seif Msangi Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji,amesema kuwa miongoni mwa athari kubwa zilizosababishwa na maafa hayo ni pamoja na nyumba kuezuliwa,Vifaa pamoja na vyakula kuharibika,na kuacha uharibifu mkubwa mali na makazi ya wananchi hao.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Wananchi Diwani wa Kata hiyo Mh.Frank Mwananziche amesema anamshukuru Mh.Mkuu wa Wilaya na wadau kwa ujumla kwa msaada walioutoa kwani utawasaidia wananchi wake katika kipindi hiki kigumu na kuomba wadau wengine kujitokeza kutoa msaada Zaidi ya hali na mali.

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MVOMERO KUENDELEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA GoT-HoMIS KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

    May 09, 2025
  • MOROGORO YAJA NA MKAKATI KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAFANYAKAZI

    May 01, 2025
  • DC NGULI ATIMIZA AHADI YA KUGHARAMIA MATIBABU YA KIJANA RAMADHANI MOHAMED

    April 28, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUWAPUUZA WANAOCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI

    April 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.