• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

MKUU WA WILAYA APIGA MARUFUKU WATENDAJI KUTEMBEA NA MIHURI

Posted on: October 13th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amepiga marufuku tabia ya Watendaji wa Kata na Vijiji , Wenyeviti wavijiji kuzunguka na mihuri kwani utaratibu huo ni kinyume na sheria na kwamba mtedanji yoyote atakayebainika kuendelea na utaratibu huo , hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara alizofanya katika tarafa ya Turiani ili kujiridhisha matumizi sahihi ya fedha za Serikali zinazoletwa kwenye miradi ya maendeleo katika shule, zahanati , vituo vya afya na miradi mbalimbali ya ujenzi katika Wilaya ya  Mvomero.. Aliongeza kuwa amebaini kuwa mihuri mingi inatumika kinyume na utaratibu na kwamba tabia hiyo inawanyima wananchi wengi haki yao.

Katika hatua nyingine , Mkuu wa Wilaya ametembelea na kufanya ukaguzi katika Shule za Sekondari Kweuma, Lusanga na kukagua ukamilishwaji wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Difinga ambazo zote zimepata ufadhili wa mradi wa BOOST unaofadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji dhahabu Barrick. Pia Mkuu wa Wilaya ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Kaole , Kata ya Kanga.

Katika ukaguzi huo, amewaasa wasimamizi wa miradi hiyo waongeze kasi ya ujenzi kwani shule hizi zinategemea kuchukua wanafunzi wanaopata adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta elimu na ni vizuri kuwatendea haki wanafunzi hao kwa kuwasogezea huduma mapema.

Akijibu swali la mwananchi aliyegusia changamoto ya upatiknaji wa mawasiliano katika Kijiji cha Difinga, Mkuu wa Wilaya amewahakikishia wananchi hao kuwa tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliona hilo na tayari ameingia mkataba wa ujenzi wa minara 758 ambapo mchakato wake ukikamilika vijiji vyote vyenye changamoto vitaweza kufikiwa na mawasiliano.

Awali katika ziara yake Mhe. Mkuu Wilaya alifika kukagua ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Luwamba Kata ya Mhonda ambao unategemewa kusambaza maji katika vijiji vingi vya Tarafa ya Turiani na kuwaondolea adha wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma hiyo muhimu katika kaya zao.

Huu ni muendelezo wa ziara za kikazi ambazo Mkuu wa Wilaya amejiwekea kila wiki kuwafikia wananchi na kukagua shughuli za maendeleo ambazo Serikali imekuwa ikileta fedha kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MKUTANO WA BARAZA LA KATA ROBO YA PILI OKTOBA - DISEMBA 2025/2026

    January 29, 2026
  • FURSA ZA UWEKEZAJI ISIWE CHANZO CHA MIGOGORO YA MIPAKA YA VIJIJI, VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMA IMARA KUIMALIZA

    January 28, 2026
  • MIPANGO, BAJETI ZA HALMASHAURI ZIENDANE NA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 - RC MALIMA

    January 27, 2026
  • DC MVOMERO ALIPONGEZA SHIRIKA LA SAWA KUJENGA MADARASA YA SHULE SHIKIZI, AAGIZA MCHAKATO WA USAJILI UANZE MARA MOJA

    January 23, 2026
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.