Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Januari 22, 2026 wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika sekta za afya na elimu, ikiwa ni sehemu ya jukumu lake la kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na miradi inakamilika kwa ubora unaotakiwa.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Koila Korman Majuka amesema ukaguzi huo unalenga kutathmini hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo, changamoto zilizopo pamoja na kutoa maelekezo ya kuboresha utekelezaji ili wananchi wanufaike na huduma bora za afya na elimu.


Katika sekta ya afya, kamati imekagua mradi wa ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Vitonga mbapo Serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni 63,755,910. Zahanati hiyo inatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi wapatao 2112 ambao wamekuwa wakilazimika kutembea umbali wa kilometa 6 kufuata huduma ya Afya katika kituo cha Afya cha Mlali.



Kwa upande wa sekta ya elimu, kamati imetembelea mradi wa ujenzi shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Mkindo shilingi milioni 528, ujenzi wa shule ya msingi WamiDakawa shilingi milioni 291, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo milioni 66 katika shule ya msingi Mkuyuni na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa kupitia mapato ya ndani milioni 25 shule hiyo ya msingi Mkuyuni.




Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Homboza kwa nguvu za wananchi huku Kamati hiyo ikitoa wito kwa wananchi kujitoa kuchangia kuendeleza ujenzi huo na kuahidi kuwa shule hiyo itajengwa.




Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.