Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero Ndg. Said Nguya ametembelea mgodi wa dhahabu uliopo katika Kijiji cha Mlandizi, Kata ya Mangae kwa lengo la kujionea shughuli za uchimbaji zinazofanyika pamoja na kusikiliza changamoto na mafanikio ya wachimbaji wa eneo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Katibu Tawala huyo amewataka wachimbaji pamoja na uongozi wa eneo hilo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji madini, kuzingatia usalama kazini pamoja na kulinda mazingira ili shughuli zao ziwe endelevu na zenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.


Katika ziara hiyo Ndg. Said Nguya ameambatana na Mkagusi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Mkoa wa Morogoro Bw. Phillipo Mathayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Dkt. Phillipina Phillipo, Mkuu wa Idara ya Maliasili na Mazingira Bi. Mary Kayowa, Afisa Biashara na Afisa Ardhi.

Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.