Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh.Suleman Jafo (MB) leo 11/12/2017 amefanya ziara Wilayani Mvomero na kukagua miradi ya maendeleo ikiwamo Hospitali ya Wilaya,Kituo cha kilimo na mifugo,Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine na Sikimu ya Umwagiliaji ya Wami Luhindo .
Akizungumza na waandishi wa Habari katika majumuisho ya ziara Mh.Suleman Jafo amesema ''Nimefurahishwa mno na hali ya usimamizi wa miradi uliofanywa na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kumtaka katibu Tawala wa Mkoa kuwaambia Wilaya nyingine waje wajifunze Mvomero''
Jafo alisema hayo alipofanya ziara ya kikazi wilayani hapa ambapo alifanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwa ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya ya sokoine,Kituo cha Kilimo na Mifugo,ujenzi wa barabara ya lami pamoja na Sikimu ya umwagiliaji ya Wami Luhindo.
Katika ziara hiyo Mh.Jafo ameagiza kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mvomero,ifikapo tarehe 13/12/2017 wakati serikali ikitafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji,Maabara,Wodi ya watoto na Majengo mengine ambayo yatagharimu zaidi ya Shilingi milioni mia saba za kitanzania (700,000,000) ambazo zitakamilisha ujenzi huo hadi kufikia mwaka 2018.
Pia Mh.Jafo ameagiza kuongezeka kasi ya kukamilisha madarasa,bwalo la chakula na mabweni katika shule ya sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine kabla ya mwezi Aprili 2018 ili shule hiyo ianze kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.