Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi - Muungano na Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina ameshiriki usafi na wananchi wa Wilaya ya Mvomero akiwemo Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mohamed Utaly pamoja na watendaji na watumishi waliomo kwenye Wilaya hiyo Jumamosi ya Tarehe 30 mwezi wa Septemba .
Mheshimiwa Luhaga alishiriki zoezi hilo kwenye eneo linaloizunguka Hospitali Kuu ya Wilaya hiyo ambayo inategemea kuzindukiwa hivi karibuni kuhudumia wananchi wa Mvomero ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata adha ya huduma za kiafya na kimatibabu.
Amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi wa Wilaya hiyo ukiongoza na Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzo Mtendaji na kuhimiza upandaji wa miti huku akihimiza mamlaka husika zisimamie zoezi hilo.
Amewataka wananchi kuunga mkono mpango wa Raisi Dkt. John Pombe Magufuli wa kushiriki usafi kila Jumamosi na zaidi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuweka mazingira safi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko pia kutunza afya za wananchi.
Hata hivyo Mheshimiwa Mpina amehoji ni kwa nini wananchi bado wanalegalega kuunga mkono jitihada za Raisi kuwataka washiriki usafi na pia kuhoji kwa nini hatua hazichukuliwi dhidi ya wananchi wanaozembea kufuata agizo hili.
Vilevile amewapa salamu kutoka kwa Raisi Dokta John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Raisi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuwataka kushiriki usafi na kwamba wanatambua kama Naibu Waziri leo yupo Mvomero.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Mohamed Utaly amewashukuru wananchi pamoja na watendaji walioshiriki kwenye zoezi hilo na kuwataka kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Raisi katika kufanya usafi na kutunza mazingira.
Naye Afisa Mazingira wa Wilaya hiyo Habib Ismail alitoa taarifa ya hali ya usafi na mazingira wilayani humo na kuwaasa wananchi kuzingatia kanuni za usafi na mazingira na vilevile kukazia kilichozungumzwa hapo awali na waliomtangulia.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.