Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwl. Mohamed Utaly kuhakikisha anawahamasisha viongozi katika ngazi ya Wilaya kuwa na mashamba darasa ya kilimo cha pamba.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo hivi karibuni katika kjiji cha Makuyu kilichopo kata ya Mvomero wilayani Mvomero alipofanya ziara maalum ya kuhamasisha wananchi kujihusisha na kilimo cha zao la pamba.
Akizungumza na wananchi hao, Dkt. Kebwe amesema kwa sasa wananchi wanapaswa kuanza kulima kilimo cha zao la pamba kama zao la biashara.
Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alifanya ziara katika Wilaya zote za mkoa huo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuanza kulima kilimo cha zao la pamba kama zao la biashara.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.